Luis Enrique ambaye alitangaza kuondoka Barcelona mapema
mwaka huu hajapata mualiko kutoka kwa Messi mpaka sasa huku kocha mpya
wa Barcelona,Erlnest Valvarde na wachezaji wote wa Barcelona wakipata
mualiko.

Kocha wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique na Messi
Awali kulikuwa na tetesi kuwa beki wa Barcelona, Gerard
Pique hataalikwa kwenye harusi hiyo baada ya kuvuja taarifa kuwa mke
wake, Shakira haziivi na mke wa Messi ambae ni mwanamitindo maarufu nchi
Hispania.
Sherehe za harusi hiyo zitafanyika katika hoteli ya
Pullman ambayo tayari vyumba 250 vimelipiwa na baadhi ya majina ya
wageni waalikwa yamekuwa siri.

Messi akiwa na mshonaji wa suti yake ya harusi, Gianni Marigliano.
Taarifa nyingine zimeeleza kuwa jumla ya watu 21 kutoka
katika timu yake ya taifa akiwemo Aguero tayari wamelikwa na maandalizi
ya harusi hiyo ya kifahari yameshaanza.
.
Comments
Post a Comment