Skip to main content

UMOJA WA VIJANA CUF WAMJIA JUU MTATIRO NA KAMATI YAKE.............//

JUMUIYA za Vijana wa Chama cha Wananchi ( CUF) katika mkoa wa Dar es Salaam, wameibuka na kulaani tabia ya inayojiita Kamati ya Uongozi ya chama hicho inayoongozwa na Julius Mtatiro, kutoa lugha za kubeza dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.

Vijana hao wamedai hatua hiyo ya Mtatiro na wenzake, kutumia vyombo vya habari hasa redio na televisheni, kumkashifu Msajili wa vyama kwa maamuzi yake ya kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kama mwenyekiti halali wa chama hicho kwa mujibu wa katiba, haikubaliki.JUMUIYA za Vijana wa Chama cha Wananchi ( CUF) katika mkoa wa Dar es Salaam, wameibuka na kulaani tabia ya inayojiita Kamati ya Uongozi ya chama hicho inayoongozwa na Julius Mtatiro, kutoa lugha za kubeza dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.

Vijana hao wamedai hatua hiyo ya Mtatiro na wenzake, kutumia vyombo vya habari hasa redio na televisheni, kumkashifu Msajili wa vyama kwa maamuzi yake ya kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kama mwenyekiti halali wa chama hicho kwa mujibu wa katiba, haikubaliki.Viongozi wa vijana wa chama hicho katika wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni, wakizungumza na waandishi wa habari jana, walimtaka Mtatiro kuacha kuwakashifu viongozi hao vinginevyo wataomba uongozi kuwachukulia hatua kulingana na Katiba ya chama ikiwemo kuondolewa uanachama.

Akisoma taarifa ya upotoshaji unaofanywa na wanaojiita Kamati ya Uongozi wa chama hicho, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa chama hicho wilaya ya Ilala, Canal Shughuly, alisema Katiba ya chana hicho inaamini kwamba kila mtu ana wajibu wa kuheshimu utu, uhuru na haki za wengine pamoja na kutii sheria halali za nchi.

Shughuly aliongozana na Katibu wa Vijana wa chama hicho Ilala, Abdul Komesha na Katibu wa Kinondoni, Yusuph Kitogota alisema kitendo cha kubezwa kwa msajili pamoja na maamuzi yake wakati anatambulika kikatiba ni kuonesha jinsi alivyo mbumbumbu wa kuielewa katiba ya chama anachokiamini.

Alisema Mtatiro ni miongoni mwa vijana waliopata bahati ya kushika nafasi ya juu ya uongozi wa ndani ya CUF ya Naibu Katibu Mkuu bara ambayo aliteuliwa na Lipumba, lakini uteuzi huo ulitenguliwa baada ya kukubwa na kashfa ya ubadhirifu wa Sh milioni 86 kwa ajili ya ununuzi wa bendera na vifaa vingine vya chama.


Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

BWANA KELVIN NOVAT ATEULIWA KUWA AFISA MAHUSIANO MPYA.

Afisa mahusiano mpya  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji AJTC Arusha, bwana Kelvin novat amesema kuwa katika kazi yake hiyo aliyoachiwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana Salum Juma Langa ataifanya kwa ufasaha kama inavyo takiwa. Afisa huyo mpya aliyetuuliwa mapema jana na bodi ya radiokatika chuo hicho  na kutangazwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana salum juma lanaga amesema kuwa hana shaka na utendaji wa kazi yake. bodi hiyo ya radio imemteua Bwana Kelvin novat kwa kipindi cha muda mfupi mpaka hapo Afisa huyo wa awali atakaporudi baada ya  kutoka likizo ya muda mfupi hapo mwezi septemba mwaka huu. sambamba na hayo Bwana kelvin amesema kazi hiyo ameyopewa sio ngeni kwake kwani alishawahi kuifanya hata kabla ya kuja chuoni hapa jambo linalomfanya kumpa motisha juu ya utendaji wa kazi yake. Afisa huyo mpya alieteuliwa kwa muda licha ya yeye kuwa na uwezo na uzoefu na kazi hiyo amesema pia anaitaji ushirikiano na wanafunzi chuoni hapo ili kuepuka kusum...

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 20 2016

Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.  Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.  Wakati huo huo , Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ...