Skip to main content

Posts

KOMBORA JINGINE LA KOREA YA KASKAZINI LAFELI KATIKA MAJARIBIO.Bofya picha hii kusoma yote

Rais wa Marekani Donald Trump ameishtumu Korea kaskazini kwamba imeikosea heshima China, mshirika wake mkuu, kwa kufyatua kombora la tatu katika kipindi cha mwezi mmoja. Kwenye ujumbe wa Twitter, bwana Trump amemsifu rais wa Uchina, Xi Jinping. Maafisa wa Marekani na Korea Kusini wanasema jaribio hilo lilitibuka, kwani kombora hilo lilianguka punde tu baada ya kupaa angani. katika mkutano wa baraza la usalama la umoja wa mataifa, Rex Tillerson, ameonya kwamba huenda kukaibuka majanga mabaya sana iwapo miradi ya Kim Jong Un ya kutengeneza zana za kinyuklia na makombora ya masafa marefu hiatositishwa. Maafisa wa Marekani wanasema kombora hilo lilipaa angani kwa sekunde kadhaa kabla ya kuanguka. Hii ni ishara kwamba Korea Kaskazini haina ujuzi wa kutosha kiteknolojia, ama pia huenda ikawa Marekani imepata mbinu ya kuingiilia mifumo yake ya teknolojia. Maafisa wakuu wa Korea kusini na Japan wamekashifu vikali majaribio ya hayo. Msemaji wa wizara ya mabo ya nje wa...

MSHUKIWA WA SHAMBULIO LA BASI LA DORTMUND MBARONI UJERUMANI.! Bofya picha hii.

Polisi ya Ujerumani imemtia mbaroni mwanamme Mjerumani mwenye asili ya Urusi,  anayeshukiwa kufanya mashambulizi dhidi ya basi lililokuwa likiwasafirisha wachezaji wa klabu ya Borussia Dortmund wiki iliyopita. Makomando wa polisi ya Ujerumani, kwa niaba ya ofisi mwendesha mashitaka wa shirikisho wamemkamata mtuhumiwa huyo,  mwenye umri wa miaka 28 katika mji wa Tübingen katika jimbo la Kusini Magharibi mwa Ujerumani la Baden Württenberg. Taarifa za awali kutokana na uchunguzi uliofanywa zimeonyesha kuwa mshambuliaji huyo aliyetambulishwa kwa jina la Sergej W. alitaka kunufaika na kuanguka kwa thamani ya hisa za klabu ya Borussia Dortmund, ambako alitarajia kungetokana na taarifa za mashambulizi kwenye basi iliyobeba wachezaji wa klabu hiyo. Uchunguzi umebainisha kuwa Sergej alikuwa amenunua hisa za klabu hiyo zenye thamani ya euro 78,000 kupitia mtandaoni,  akiwa katika hoteli ya klabu hiyo alikokuwa amekodi chumba kuanzia tarehe ...

PROFESA LIPUMBA ATINGA MAHAKAMANI.!

Mgororo wa ruzuku ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) unazidi kupamba moto baada ya mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kwenda kuitetea mahakamani.   Profesa Lipumba na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa chama hicho, Thomas Malima wamefungua maombi Mahakama Kuu wakiomba waunganishwe kwenye kesi iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa CUF, walio upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.   Katika kesi ya msingi ya ruzuku namba 21 ya mwaka 2017, wadai wanaiomba Mahakama imzuie msajili kutoa ruzuku kwa CUF na imuamuru Sh360 milioni alizozitoa kwa kina Profesa Lipumba zirejeshwe kwenye akaunti rasmi ya chama.  Wadaiwa katika kesi hiyo ni Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini Profesa Lipumba na Malima wamewasilisha maombi mahakamani nao waunganishwe kwenye kesi hiyo upande wa wadaiwa.   Maombi hayo yalitajwa jana na Malima aliieleza mahakama...

MAHAKAMA NCHINI URUSI YAPIGA MARUFUKU MASHAHIDI WA YEHOVA.!

Mahakama ya Juu nchini Urusi imekubali ombi la serikali kuorodhesha kanisa la Mashahidi wa Yehova, kwa Kiingereza Jehovah's Witnesses,  kama kudi la kidini lililoharamishwa, na kuliorodhesha kuwa kundi lenye msimamo mkali. Wizara ya haki nchini humo ilisema kundi hilo lilikuwa limesambaza nyaraka zilizokuwa na ujumbe wa kuchochea chuki dhidi ya makundi mengine. Mawakili waliokuwa wanatetea kundi hilo wamekanusha madai hayo na wamesema watakata rufaa. Kundi hilo la kidini lina waumini 175,000 nchini urusi, taifa ambalo wafuasi wa madhehebu hayo waliteswa na kudhulumiwa wakati wa utawala wa Josef Stalin. Inakadiriwa kwamba kuna watu milioni nane kote duniani ambao ni waumini wa madhehebu hayo ya Kikristo, yanayofahamika sana kwa kampeni zake za kwenda nyumba kwa nyumba kutafuta waumini wapya. Wafuasi wa kundi hilo la kidini wanasema hatua ya kuharamisha kundi hilo ina maana kwamba shughuli zake pia ni haramu kisheria. Wizara ya haki iliiomba mahakama kufu...

MAHAKAMA YATOA AMRI AGNESS MASOGANGE AKAMATWE.!

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamata msanii, Agnes Gerald maarufu kama Masogange kwa kushindwa kuhudhuria kwenye kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili. Hati hiyo ilitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi mkuu, Wilbroad Mashauri, wakati kesi hiyo ilipotajwa. Wakili wa Serikali, Adolf Mkini alidai mahakamani hapo kwamba upelelezi wa kesi hiyo upo hatua za mwisho, lakini mshtakiwa, wadhamini wake na wakili wake hawakufika hivyo wakili Nkini akaomba mahakama itoe hati ya kumkamata mshtakiwa huyo kwa sababu ni mara ya pili ameshindwa kufika mahakamani hapo. Hakimu Mashauri alikubali maombi ya wakili wa Serikali na kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa ambaye ni Masogange. Msanii huyo aliwahi kuonywa akitakiwa aheshimu mahakama kutokana na kutokuwapo kwenye kesi yake ilipotajwa. Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam, a...

MAREKANI: IRAN INAFANYA UCHOKOZI WA HALI YA JUU.!

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ameituhumu Iran kwa kufanya "uchokozi wa hali ya juu" unaoendelea ambao amesema unanuia kuvuruga uthabiti katika Mashariki ya Kati na kuhujumu juhudi za Marekani katika kanda hiyo. "Iran isipochukuliwa hatua inaweza kwenda njia sawa na ya Korea Kaskazini na kuubeba ulimwengu wote katika safari hiyo," Bw Tillerson amesema. Rais Donald Trump tayari ameagiza utathmini mpya ufanywe kuhusu mkataba uliotiwa saini kati ya nchi za Magharibi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran. Hata hivyo, Marekani imekiri kwamba Tehran inatii makubaliano hayo ya mwaka 2015. Iran kufikia sasa haijasema lolote kuhusu tamko hilo jipya kutoka kwa Marekani. Iran imekanusha mara kwa mara tuhuma kutoka kwa nchi za Magharibi kwamba inajaribu kustawisha silaha za nyuklia. Jumanne, Marekani iliituhumu Korea Kaskazini na kusema taifa hilo lilikuwa linajaribu kufanya "uchokozi kutokee jambo fulani", baada ya nchi hiyo kuf...

KOREA YA KASKAZINI INAAMINIKA KUMILIKI SILAHA 1000 ZENYE UWEZO TOFAUTI.!

Korea kaskazini inaaminika kumiliki zaidi ya silaha 1000 zenye uwezo tofauti ikiwemo kombora la maasafa marefu ambalo linaweza kuishambulia Marekani. Mpango wa Pyongyang umeendelea katika miongo kadhaa ya hivi karibuni kutoka mizinga mikubwa katika miaka ya tisini na sabini hadi makombora ya masafa mafupi mbali na yale ya masafa marefu katika miaka 80 na 90. Mifumo ilio na uwezo mkubwa inadaiwa kufanyiwa utafiti. Hivi karibuni, Korea Kaskazini ilitangaza kwamba inaunda makombora ya masafa marefu yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine ambayo yanaweza kushambulia mataifa ya magharibi. Taifa la Korea Kaskazini linaaminika kutengeza kombora la masafa marefu zaidi ambalo wachunguzi wamelitaja kuwa KN-08 ama Hwasong-13. Image caption Makombora ya Hwasong yakiwa katika maonyesho            ...