Skip to main content

Posts

Unyevu umegunduliwa na wanasayansi katika sayari ilio sawa na dunia.! Bofya picha hii kujua zaidi.

Wanasayansi wanasema kwa mara ya kwanza wamegundua kuna unyevu unaoizunguka sayari ilio kama dunia. Wameichunguza sayari hii inayotambulika kama GJ 1132b ambayo ukubwa wake ni zaidi ya dunia kwa mara 1.4 na iko umbali wa miaka 39 ya kasi ya muanga. Uchunguzi wao unaonyesha kuwa sayari hii imezingirwa na gesi ya methane au maji au mchanganyiko wa zote mbili. Habari hii ni muhimu sana kwa kuendeleza masomo yanayohusiana na maisha nje ya mfumo wa jua. Hata hivyo kuna uwezekano kuwa mtu hawezi kuishi katika dunia hii kwa sababu ya joto jingi la 370C. Dkt. John Southworth ni mtafiti mkuu kutoka chuo kikuu cha Keele na anasema: "Kulingana na maarifa niliyo nayo, joto la juu zaidi ambalo mwanadamu ameweza kustahimili hapa duniani ni 120C." Kugunduliwa kwa sayari ya GJ 1132b kulitangazwa kwanza mwaka wa 2015. Sayari hii iko katika mkusanyiko wa Vela, anga ya kusini. Ingawa ukubwa wake ni sawa na dunia, nyota inayozunguka ni ndogo na yenye mwanga mdogo kuliko...

United wampa mkataba mpya kinda Jesse Lingard.!

Mchezaji wa Manchester United Jesse Lingard amesaini mkataba mpya na timu yake na atakua akilipwa mshahara wa paundi 75,000 kwa wiki na kama timu yake watafuzu kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya at apata paundi 100,000 kwa Wiki. Mkataba wake huo mpya utabakisha Jesse klabuni hapo mpaka mwaka 2021 na kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka moja zaidi katika mkataba huo wa sasa. Lingard ameichezea klabu yake jumla ya michezo sabini, msimu huu amecheza michezo 29 na kufunga mabao 5 na alijiunga ma timu hiyo akiwa na umri wa miaka saba. Mchezaji huyo alianza kuchomoza chini ya meneja Louis van Gaal na kabla ya hapo alipelekwa kwa mkopo kwenye Klabu za Leicester City, Birmingham City, Brighton na Derby County.

HEALTH DAY: Zimetajwa hizi kuwa ndiyo nchi zenye wananchi wenye afya duniani.! Bofya picha hii kusoma story yote.

April 7 kila mwaka Dunia huadhimisha Siku ya Afya ambapo leo ni April 7, 2017 nimeona siyo vibaya nikikusogezea list ya nchi 25 zenye wananchi wenye afya nzuri zaidi duniani. Katika kuadhimisha Siku ya Afya Duniani 2017, Bloomberg Health Index  imeziorodhesha nchi 25 zenye wananchi waliokuwa na afya nzuri ambapo Italia  imetajwa kama kinara kwa kuwa na wananchi wenye afya na wanaoishi kwa miaka mingi hadi kufikia miaka 100.  Sierra Leone imetajwa pia kuwa miongoni mwa nchi zenye wananchi wasio na afya duniani na kwa mujibu wa list hii nchi zilizotajwa zinaongoza kwa kuwa na asilimia chache ya vifo kwa mwaka huku zikiwa na hospitali za kutosha, asilimia ndogo ya magonjwa ya kuambukiza na wananchi wake huishi miaka mingi ukilinganisha na nchi nyingine.

Marekani imeishambulia Syria kwa makombora.!

Marekani imefanya shambulizi la makombora takriban 50 ,yalipigwa katika kambi ya jeshi la anga mjini Homs nchini Syria. Awali maafisa wa Marekani walisema wana mpango wa kuchukua hatua za kijeshi baada ya Syria kushutumiwa kutumia silaha za kemikali katika mji unaodhibitiwa na waasi, ambapo watu kadhaa wamepoteza maisha. Mashambulizi hayo yametekelezwa kutoka kwenye meli za kijeshi za Marekani katika bahari ya Mediterranea. Rais wa Marekani Donald Trump amesema ameamuru kutekelezwa kwa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Syria huku akitoa wito kwa mataifa yote yaliyostaarabika kukomesha vitendo vya mauaji na umwagaji damu nchini humo Naye mshirika wa Syria Urusi ametahadharisha madhara yatokanayo na hatua zozote za kijeshi zinazochukuliwa na Marekani dhidi ya Syria . Hata hivyo Rais Donald Trump amsema kuwa ,kutumia gesi hatari kuua raia waki...

UTAFITI: Mpya kutoka kwa Wanasayansi, wamegundua tiba ya hangover.!

Hii ni dunia ambayo kila siku watu wanafanya utafiti wa mambo mbaimbali…sasa leo April 7, 2017 nakuletea matokeo ya utafiti uliofanywa na wanafunzi wa wawili nchini Marekani waliogundua tiba ya hangover. Unaambiwa katika stori iliyochapishwa na Daily Mail March 29, 2017,  wanafunzi wawili kutoka Yale University wamegundua tiba hiyo ambayo wameapa jina la SunUp  ikiwa ni unga uliotokana na mchanganyiko wa viungo vya asili ambao umegunduliwa kwa lengo la kuvunja vunja molikuli za sumu kwenye ini , na kubalansi glutamine  pamoja na kuuamsha mwili kwa elektroliti baada ya kunywa pombe. Margaret Morese na Liam McClintock ambao waliathiwa sana na hangover  waligundua tiba hiyo baada ya kujaribu viungo vya asili kila kimoja kivyake katika tafiti huru kuthibitisha uwezo wake dhidi ya kuondoa athari za kilevi na ulinzi thabiti dhidi ya sumu itokanayo na kilevi kwa mtumiaji na baadaye kutengeneza unga huo ambao humtaka mtumiaji kuuchanganya kwenye maji ...

Ujerumani, Poland na England zajiimarisha.!

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Löw alikamilisha kazi yake baada ya mabingwa hao wa dunia kupata ushindi watano kwenye mechi tano katika Kundi lao la kufuzu Kombe la Dunia. Ushindi wao wa 4-1 dhidi ya Azerbaijan mjini Baku ulikuwa suala rahisi tu kwa Wajerumani ambao walifungwa bao lao la kwanza kabisa katika Kundi C.  Ujerumani wanaongoza kileleni na pengo la pointi tano dhidi ya Ireland ya Kaskazini ambayo iliizaba Norway 2-0.  Nayo Jamhuri ya Czech iliizaba San Marino 6-0. England ilipambana na kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Lithuania. Ni mechi ambayo mshambuliaji Jermain Defoe mwenye umri wa miaka 34 alirejeshwa kikosini na akafunga bao lake la 20 la kimataifa.  England sasa imejiimarisha kileleni mwa Kundi F. Vijana hao wa kocha Garry Southgate sasa ndio timu pekee ya Ulaya ambayo haijafungwa bao hata moja kufikia sasa.  England wana pointi 13, nne mbele ya Slovakia ambao walisonga katika nafasi ya pili ya kundi hilo kwa ...

Matumizi ya silaha za sumu Syria kuchunguzwa.! Bofya picha hii kupata story nzima.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mashambulizi yanayotuhumiwa kuwa ya silaha za sumu yaliofanyika nchini Syria hapo Jumanne yanapaswa kuchunguzwa. Kauli ya Guterres inakuja wakati kundi linalofuatilia hali ya Syria likisema idadi ya vifo kutokana na mashambulio hayo ya Jumanne katika mji wa kaskazini imeongezeka na kufikia 72, na wanaharakati pia wameripoti kurudiwa kwa mashambulizi ya anga katika mji huo. Guteress amewaambia waandishi wa habari leo hii katika mkutano wa wafadhili wa Syria unaofanyika Brusels kwamba anataraji wakati huu utaweza kuimarisha uwezo wa wale ambao wana wajibu katika hali hiyo. Amesema matukio hayo ya kutisha yanaonyesha uhalifu wa kivita ukiendelea kutendeka nchini Syria na kwamba sheria ya kimataifa inaendelea kukiukwa mara kwa mara.Ameongeza kusema ana imani kwamba Baraza la Usalama litatimiza wajibu wake wakati litakapokutana baadae leo hii. Baraza la Usalama kujadili mashambulizi hayo Marekani, Ufarans...