Barcelona watawapa Liverpool pauni
milioni 120 za kumsajili Philippe Coutinho, 25, baada ya Neymar, 25,
kwenda Paris Saint-Germain. (Star)
Barcelona wanaweza kutumia fedha walizopata za mauzo ya Neymar kwa kumsajili kiungo mshambuliaji wa PSG Julian Draxler, 23, ambaye wakala wake ameonekana katika mitaa ya Barcelona. (Bild)
Antonio Conte anamtaka beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, na pia ameitaka bodi ya Chelsea kufanya usajili zaidi baada ya kuona kikosi chake kikifungwa na Arsenal. (Daily Mirror)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp yuko tayari kuacha kumfuatilia Virgil van Dijk, na badala yake kuwaamini mabeki aliokuwa nao sasa. (Mirror)
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema wachezaji zaidi wataondoka Emirates kabla ya dirisha la usajili kufungwa kwa sababu kikosi chake ni kikubwa mno. (Telegraph)
Barcelona wamekubaliana na mshambuliaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, 20, lakini sasa wanahitaji kukubaliana ada ya uhamisho ambayo Dortmund wamesema wanataka pauni milioni 90.2. (L'Equipe)
Barcelona wapo kwenye mazungumzo ya kutaka kumsajili kiungo wa zamani wa Tottenham Paulinho, 29, kutoka Guanghzhou Evergrande ya China. (Sport)
Chelsea wapo tayari kupambana na Manchester United katika kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 28, ambaye atagharimu takriban pauni milioni 90. (Express)
Chelsea, Manchester United na Monaco zinamtaka beki wa Barcelona Sergi Roberto, 25, ambaye anaweza kuuzwa kwa pauni milioni 36.1. (Don Balon)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameutaka utawala wa klabu yake kumsajili beki wa kulia wa Monaco, Fabinho, 23. (Don Balon)
Baada ya Nemanja Matic kwenda Manchester United kinyume na matakwa yake, meneja wa Chelsea Antonio Conte amekiri kuwa hawezi kuzuia uuzwaji wa Eden Hazard, 26, ambaye ananyatiwa na Barcelona. (Star). BBC
Comments
Post a Comment