Skip to main content

KUELEKEA MCHEZO WA REAL VS UNITED, HIZI NDIO TAKWIMU NA RECORDS ZA UEFA SUPER CUP.

Msimu mpya wa soka barani Ulaya unatarajiwa kuanza rasmi leo wakati utakapopigwa mtanange utakaowakutanisha wababe wa ulaya msimu uliopita. Mabingwa wa Champions League Real Madrid na mabingwa wa Europa Cup Manchester United.

Mchezo huu utapigwa nchini Macedonia mashariki mwa bara la ulaya, kuanzia majira ya 9:45 usiku.
Mchezo huu unakutanisha miamba mikubwa ya soka barani ulaya siku chache baada ya kukutana nchini Marekani katika mechi za maandalizi ya msimu mpya. 


Cristiano Ronaldo amerejea mazoezini wiki iliyopita na leo ametajwa katika kikosi kinachosafiro kuelekea Macedonia kwa ajili ya mchezo huo, United watamkosa Eric Bailly pamoja na Phil Jones wenye adhabu za kufungiwa mechi kutokana na makosa ambayo waliyatenda msimu uliopita.


Kwa kuanzia kuuchambua mchezo huu tuanze kuangalia takwimu mbalimbali zinazohusisha mchezo wa UEFA Super Cup tangu ulipoanzishwa kuchezwa mnamo mwaka 1973.

Champions League vs UEFA Cup Winners
• Mabingwa wa Champions League wameshinda kombe hili mara 22 kati ya mara 41.
• Mabingwa wa UEFA Cup/UEFA Europa League wameshinda kombe hili mara 7 kati ya 17 tangu lilipokufa kombe la Washindi (UEFA Cup Winners' Cup.)

Mataifa yaliyoshinda mara nyingi
13: Spain 🇪🇸 wameshinda kombe hili mara 13 kupitia vilabu vyao (Barcelona 5, Real Madrid 3, Valencia 2, Atlético Madrid 2, Sevilla 1)

9: Italy 🇮🇹 wameshinda Super Cup mara 9 kupitia vilabu vyao (AC Milan 5, Juventus 2, Lazio 1, Parma 1)
7: England wanafuatia kwa kushinda mara 7 (Liverpool 3, Aston Villa 1, Chelsea 1, Manchester United 1, Nottingham Forest 1)

Vilabu vilivyoshinda UEFA Super Cup mara nyingi
5: AC Milan, Barcelona
3: Liverpool, Real Madrid
2: Ajax, Anderlecht, Atlético Madrid, Juventus, Valencia

Mchezaji aliyeshinda Super Cup Mara nyingi
4= Dani Alves (Sevilla 2006, Barcelona 2009, 2011, 2015)
4= Paolo Maldini (AC Milan 1989, 1990, 1994, 2003)


Kocha aliyeshinda mara nyingi
3= Carlo Ancelotti (AC Milan 2003, 2007, Real Madrid 2014)
3= Josep Guardiola (Barcelona 2009, 2011, Bayern München 2013)


Nchi zilizoshiriki mchezo wa Super Cup mara nyingi
25: Spain wameshiriki mara 25 kupitia vilabu vya (Barcelona 9, Real Madrid 6, Sevilla 5, Valencia 2, Atlético Madrid 2, Real Zaragoza 1)

16: Waingereza 🇬🇧 wameshiriki mara 16 kupitia vilabu vya (Liverpool 5, Manchester United 4, Chelsea 3, Nottingham Forest 2, Arsenal 1, Aston Villa 1)
13: Italy mara 13 (AC Milan 7, Juventus 2, Internazionale Milano 1, Parma 1, Lazio 1, Sampdoria 1)
Vilabu vilivyoshiriki mara nyingi
9: Barcelona
7: AC Milan
6: Real Madrid
5: Liverpool, Sevilla
4: Bayern München, Porto, Manchester United

Mchezo uliokuwa na idadi kubwa ya magoli : 2015, Barcelona 5-4 Sevilla
Ushindi mkubwa zaidi *: 2006, Sevilla 3-0 Barcelona, na mtanange wa 2012 kati ya Atlético Madrid 4-1 Chelsea
Rekodi binafsi
Goli la haraka zaidi: Éver Banega (Dakika 3 – 2015: Barcelona 5-4 Sevilla)

Waliofunga Hat-tricks: Radamel Falcao (2012, Atlético Madrid v Chelsea) na Terry McDermott (1977, Liverpool v Hamburg)

Waliofunga magoli ya kujifunga: Patrick Paauwe alijifunga goli pekee katika historia ya Super Cup kwenye mchezo wa kipigo cha Feyenoord cha mabao 3-1 kutoka kwa Real Madrid mwaka 2002.

Waliopata kadi nyekundu: Wachezaji wanne wameshapata kadi nyekundu kwenye mchezo wa Super Cup – Paul Scholes (2008, United), Rolando na Fredy Guarín (2011, Porto) na Thimothée Kolodziejczak (Sevilla, 2016).

Wachezaji waliocheza mechi nyingi za UEFA Super Cup **
8: Alessandro Costacurta (AC Milan), Roberto Donadoni (AC Milan)
7: Paolo Maldini (AC Milan), Daniele Massaro (AC Milan), Mauro Tassotti (AC Milan)
6: Franco Baresi (AC Milan), Arie Haan (Ajax, Anderlecht)
5: Dani Alves (Sevilla, Barcelona), Marcel Desailly (AC Milan, Chelsea), Albert Ferrer (Barcelona, Chelsea), Ronald Koeman (PSV Eindhoven, Barcelona), Attilio Lombardo (Sampdoria, Juventus, Lazio), Phil Neal (Liverpool)


Wafungaji bora wa UEFA Super Cup
3: Oleh Blokhin (Dynamo Kyiv), Radamel Falcao (Atlético Madrid), Arie Haan (Ajax, Anderlecht), Terry McDermott (Liverpool), Lionel Messi (Barcelona), Gerd Müller (Bayern München), Rob Rensenbrink (Anderlecht), François Van der Elst (Anderlecht

**UEFA Super Cup ulikuwa unachezwa kwa mfumo wa mechi za nyumbani na ugenini kuanzia mwaka 1973 mpaka 1997. DAUDA

Comments

Popular posts from this blog

Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi.!

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani. Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani.  Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine. 7: Rand – Afrika Kusini (1$=14) Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14. 6: Pula – Botswana (1$ = 10.8) Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokana...

BWANA KELVIN NOVAT ATEULIWA KUWA AFISA MAHUSIANO MPYA.

Afisa mahusiano mpya  katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji AJTC Arusha, bwana Kelvin novat amesema kuwa katika kazi yake hiyo aliyoachiwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana Salum Juma Langa ataifanya kwa ufasaha kama inavyo takiwa. Afisa huyo mpya aliyetuuliwa mapema jana na bodi ya radiokatika chuo hicho  na kutangazwa na aliyekuwa afisa mahusiano bwana salum juma lanaga amesema kuwa hana shaka na utendaji wa kazi yake. bodi hiyo ya radio imemteua Bwana Kelvin novat kwa kipindi cha muda mfupi mpaka hapo Afisa huyo wa awali atakaporudi baada ya  kutoka likizo ya muda mfupi hapo mwezi septemba mwaka huu. sambamba na hayo Bwana kelvin amesema kazi hiyo ameyopewa sio ngeni kwake kwani alishawahi kuifanya hata kabla ya kuja chuoni hapa jambo linalomfanya kumpa motisha juu ya utendaji wa kazi yake. Afisa huyo mpya alieteuliwa kwa muda licha ya yeye kuwa na uwezo na uzoefu na kazi hiyo amesema pia anaitaji ushirikiano na wanafunzi chuoni hapo ili kuepuka kusum...

Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 20 2016

Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. Uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.  Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.  Wakati huo huo , Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.  Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Katika hatua nyingine , Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ...