Aliyekuwa meneja wa zamani wa Diamond, Rich Mavoko, Nay wa Mitego pamoja na wasanii wengine, Meneja Maneno, amefunguka kwa kutaja majina ya baadhi ya wasanii anaodai wanaamini ushirikina huku akikiri kuna wasanii wengine ambao yeye mwenyewe aliwapeleka kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kuroga. Meneja Maneno amedai Rich Mavoko, Sam wa Ukweli ni moja kati ya wasanii wanaoamini ushirikina huku akidai katika wote Diamond Platnumz ndiyo zaidi yao. “Ndele ni sehemu ambayo baadhi ya wasanii waliiamini sana lakini Mungu akisema ‘Yes’ ni ‘Yes’ tu kwa hiyo nakumbuka wasanii ambao nilikwenda nao kwa waganga kuroga ni pamoja na Rich Mavoko tena tulienda mbali kabisa huko Kigamboni ndani ndani huko tumeenda ndugu yangu, nilisharusha nazi katikati yaani usiku ule unajifanya chizi kama umevurugwa,” Meneja Maneno alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio. Meneja Maneno Aliongeza, “Hata Sam wa Ukweli siwezi kukataa, ni watu ambao imani yao iliw...