Skip to main content

Posts

MOURINHO AWASILI URENO LEO KWA MAZISHI YA BABA YAKE MZAZI.! Bofya picha hii kuona picha zaidi.

Jose Mourinho na Baba yake mzazi Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho tayari ameshafika nchini Ureno kwa ajili ya mazishi ya baba yake mzazi. Baba yake huyo aitwae Jose Manuel Mourinho Felix 79 amefariki Dunia wikiendi iliyopita baada ya kuugua kwa muda mrefu na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo huko jijini Setubal nchini Ureno. Mapema jana Mourinho kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka picha ya baba yake huku ikiwa na rangi nyeusi na nyeupe (B&W) na hakuandika kitu huku maoni ya mashabiki wakionekana kumpa pole kwa msiba uliompata. Katika enzi za uhai wake Baba mzazi wa Mourinho alishawahi kuitumikia timu ya taifa ya Ureno na Klabu ya Victoria Setubal FC kwa michezo 250.    Hapa nimekuwekea picha za Mourinho alivyowasili Ureno kwa kwa ajili ya mazishi ya baba yake mzazi. Mourinho akipokelewa na baba yake mdogo mapema leo Mtoto wa kike wa Mourinho wa pili kulia, nae alikuwepo kwenye mapokezi ya baba yake mzazi Mourinho na Binti yake w...

GOOGLE YAPIGWA FAINI YA DOLA BILION 2.7 KWA KUKIUKA SHERIA ZA MAUZO. !

Google imepigwa faini ya ya dola bilioni 2.7 na tume ya ulaya baada ya tume hiyo kuamua kuwa Google ilikuwa imekiuka mamlaka yake ya kuweka matangazo yake binafasi kuwa ya kwanza. Faini hiyo ndiyo kubwa zaidi iliyotolewa na tume ya ulaya hadi leo, kwa kampuni ambayo imelaumiwa kwa kukiuka sheria za biashara. Amri hiyo pia inataka Google kundoa vizingiti vinavyozuia ushindani ndani ya kipindi cha siku 90 la sivyo ichukuliwe hatua zaidi. Haki miliki ya picha EUROPEAN COMMISSION Image caption Margrethe Vestager alisema kile ambacho Google imekifanya na haramu chini ya sheria za EU Kampuni hiyo ya Marekani inasema huenda ikakata rufaa. Tume ya Ulaya ilisema inaiachia Google jukumu la kuamua ni mabadiliko yapi itafanyia mifumo yake ya mauzo. "Kile ambacho Google imekifanya na haramu chini ya sheria za EU," alisema Margrethe Vestager, kamishina wa ushindanii wa kibiashara wa tume ya EU. Haki miliki ya picha Image caption Matangazo huyasukuma mengine nje hasa kwenye si...

MICHUANO YA CONFIDARATION CUP NI PATASHIKA LEO URUSi !. Bofya picha hii .

Michuano ya mabara almaarufu kama Confedaration Cup inaanza kutimua vumbi nchini Russia hii leo kwa wenyeji Russia watakaoikaribisha New Zealand katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo. Mchezo huu kati ya Russia na NewZealand unatarajiwa kupigwa katika dimba la St Petersburg uwanja wa nyumbani wa klabu ya St Petersburg huku Winston Reid mlinzi wa West Ham na timu ya taifa ya New Zealand akikosa mechi hiyo kutokana na majeraha. Timu ya taifa ya Ureno wataliwakilisha bara la Ulaya kama mabingwa wa bara hilo huku waandishi wa habari wakiwa wamepiga kambi katika timu hiyo kufuatilia mkasa mkubwa wa kodi unaomuandama Ronaldo. Andre Silva mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno amewaambia waandishi wa habari kwamba “Ronaldo anaichukulia michuano hii serious sana na hawazi yanayotokea nje ya uwanja bali akili yake yote iko katika michuano hii” Toka suala la Ronaldo kudaiwa kukwepa kodi lianze kutawala vyombo vya habari inasemekana Mreno huyo hana raha na anafikiria kuondoka nch...

KING-LEO MESSI AAPA KUSALIA BARCELONA HADI TAMATI.! Bofya picha hii

Lionel Messi alifunga magoli manne katika mechi ya fainali ya Copa del Rey, na kuwa mchezaji wa kwanza tangu mchezaji wa Athletic Bilbao Telmo Zarra kufanya hivyo mwaka 1950. Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amesema angependa kusalia na klabu yake kwa siku zilizosalia katika taaluma yake. ''Ni kitu ambacho nimekuwa nikikitazamia na ni kitu nilichokuwa nikikitaka," alisema. Kiungo huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na Barcelona akiwa na umri wa miaka 13, akashiriki mechi yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 17 na amefunga zaidi ya magoli 500 akiwa na klabu hiyo. Messi ameshinda taji La liga mara nane, Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara nne na tuzo mchezaji bora duniani Ballon d'Or mara tano. Msimu uliopita chini ya kocha Luis Enrique, Barcelona walikuwa katika nafasi ya pili kwa ligi ya La Liga, alama tatu chini ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Real Madrid. Walishindwa 3-0 katika robo fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya...

FAINALI YA NBA;GOLDEN STATE WORRIORS YAENDELEA KUINYANYASA CAVALIERS.Bofya picha hii.

Golden State Warriors imeendelea kuinyanyasa Cleveland Cavaliers katika fainali ya tatu ya mchezo wa kikapu wa NBA.   Katika mchezo huo uliochezwa alfajiri ya kuamkia leo katika uwanja wa Quicken Loans Arena, Golden wameshinda kwa jumla ya vikapu 118 dhidi ya 113 vya Cleverland. Mchezaji Kevin Durant ameendelea kuwa nyota wa fainali hizo baada ya kufanikiwa kushinda pointi tatu zikiwa zimebakia sekunde 45 za mchezo huo kumalizika. Kwa sasa unasubiriwa mchezo wa mwisho utakaochezwa wikiendi hii ambapo kama Golden atashinda tena ndio atakuwa bingwa mpya wa mchezo huo kwa mwaka huu ambao msimu uliopita ulinyakuliwa na Cleveland Cavaliers.

LUIZ ENRIQUE,SHAKIRA NA PIQUE WAIKOSA HARUSI YA KING LEO-MESSI.Bofya picha hii

Luis Enrique ambaye alitangaza kuondoka Barcelona mapema mwaka huu hajapata mualiko kutoka kwa Messi mpaka sasa huku kocha mpya wa Barcelona,Erlnest Valvarde na wachezaji wote wa Barcelona wakipata mualiko.                            Kocha wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique na Messi   Awali kulikuwa na tetesi kuwa beki wa Barcelona, Gerard Pique hataalikwa kwenye harusi hiyo baada ya kuvuja taarifa kuwa mke wake, Shakira haziivi na mke wa Messi ambae ni mwanamitindo maarufu nchi Hispania.   Sherehe za harusi hiyo zitafanyika katika hoteli ya Pullman ambayo tayari vyumba 250 vimelipiwa na baadhi ya majina ya wageni waalikwa yamekuwa siri.            Messi akiwa na mshonaji wa suti yake ya harusi, Gianni Marigliano. Taarifa nyingine zimeeleza kuwa jumla ya watu 21...

UNITED KLABU TAJIRI ZAIDI DUNIANI!

Klabu ya Manchester United imetajwa kuwa ndio timu yenye thamani kubwa duniani kwa mujibu wa jarida la habari za biashara la Forbes United inathamani ya kiasi cha pauni billion 2.86 hii ni mara ya kwanza kwa Man United kuongoza listi hiyo katika miaka mitano. BARCELONA wako katika nafasi ya pili wakiwa na thamani ya pauni bilioni 2.82, mabingwa wa ulaya Real Madrid wako katika nafasi ya tatu wakiwa na thamani ya pauni bilioni 2.77. Timu zinazofuata kwa thamani duniani             4) Bayern Munich - $2.71bn (£2.10bn)             5) Manchester City - $2.08bn (£1.61bn)            6) Arsenal - $1.93bn (£1.50bn)            7) Chelsea - $1.85bn (£1.43bn)            8) Liverpool - $1.49bn (£1.15bn)      ...