Skip to main content

Posts

Qaswida~Mwajitia Adhabuni

Inshaallah.Mungu awalipe kila la kheri katika kazi hii ya kufikisha Ujumbe wa Allah Kwa njia hii ya Qaswida.Natumai Ujumbe Umetufikia Inshaallah Tutaufanyia kazi.Mwenyezimungu NiMwingi wa rehema Nainshaallah Awaongoze katika Kazi Hii Tukufu.Inshaallah.

AZAM TV WAFANYA YAO, WAZINDUA FULL DOWZII KUTWA MARA TATU

Kituo cha Runinga kinachozidi kufanya vema kwa kasi chaAzam TV, jana Jumnne kimezundua promosheni yake mpya ya Full Dowzii Kutwa Mara Tatu ambayo itakuwa mahususi kwa ajili ya wateja wao wapya. Katika promosheni hiyo, mteja atapewa king’amuzi, dishi, rimoti na vifaa vyake vyote pamoja na kuunganishiwa king’amuzi hicho endapo mteja huyo atalipia kifurushi kikubwa cha Azam Play kwa mwaka mmoja. Mkurugenzi wa Matukio wa Azam TV, Yahya Mohamed, amesema: “kwa kawaida mteja mpya hununua king’amuzi cha Azam TV pamoja na vifaa vyake vyote kwa Sh 135,000, huku gharama za ufundi zikiwa ni Sh 30,000 ambapo jumla ni Sh 165,000. “Lakini mteja mpya ukilipia Sh 336,000 kwa ajili ya kifurushi cha Azam Play kwa mwaka, utaokoa Sh 165,000. Hivyo niwaambie tu wateja wetu Azam tumekuja kwa ajili ya kuwakomboa na kupata burudani kila siku bila ya kikomo.” Aidha, Mohamed alisema, Azam TV ina vifurushi vitatu vya mwezi ambavyo ni Azam Pure Sh 15,000, Azam Plus Sh 23,000 na...

KADI ZA TIKETI ZA ELEKTRONIKI KUTOLEWA BUREEE KABISA, WAZIRI NAPE ALIZUNGUMZIA ZOEZI

Kadi za kilektroniki kwa ajili ya kuingia uwanjani zitakuwa zikitolewa bure. Hii ni ni baada ya ya hivi karibuni serikali kufunga mashine za kielektroniki katika Uwanja wa Taifa, kadi kwa ajili ya kuingilia uwanjani humo zitatolewa bure. Serikali iliamua kufunga mashine hizo katika uwanja huo ili kuondokana na mfumo wa zamani wa kutumia tiketi za kawaida kwa lengo la kulinda mapato yake uwanjani hapo ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa yakiishia mifukoni mwa wajanja wachache. Akizungumza katika semina elekezi ya jinsi ya kutumia mfumo huo mpya wa kuingia uwanjani humo uliozinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Meneja Miradi wa Kampuni ya Selcom ambayo ndiyo iliyopewa jukumu la kusimamia mfumo huo, Gallus Runyeta amesema kuwa kadi zitakazokuwa zikitumika katika mfumo huo zitatolewa bure. Amesema kadi hizo zitaanza kutolewa hivi karibuni ambapo kutakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaofanyika katika uwanja huo ambao ser...

WABUNGE YANGA, SIMBA WAUNGANA KUCHANGIA WALIOKUTWA NA MAAFA YA TETEMEKO LA KAGERA

Wabunge wapenzi wa Simba wanatarajia kuumana wikiendi hii, ikiwa ni mechi mahsusi kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni huko mkoani Kagera. Mbali na mechi hiyo pia kutakuwa na mechi za ufunguzi baina ya Bongo Muvi dhidi ya Bongo Fleva, pia kutakuwa na mechi ya netiboli itakayoikutanisha timu ya bunge dhidi ya ile ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), mechi zote hizo zitapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar. Mbunge wa Sengerema na Mwenyekiti wa Bunge SC, William Ngeleja ameweka wazi kuwa licha ya wabunge hao kuchangia kiasi cha Sh milioni 85 kupitia posho zao wakiwa bungeni lakini bado wameona kuna msaada zaidi unahitajika kwa ajili ya angalau kurejesha hali ya maisha ya awali ya Kagera ndiyo maana kumeandaliwa mechi hizo. “Lengo letu ni kukusanya fedha za kuwasaidia ndugu zetu wa kule Kagera, angalau warejewe na hali waliyokuwa nayo awali, tangu awali kule bungeni kupitia posho zetu tulishachang...

Ndege mpya ya aina ya Bombardier Q400 NextGen iliyonunuliwa na Serikali yawasili Jijii Dar es Salaam

Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016. Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakisubiri kuwasili kwa Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016 Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikipata saluti ya maji (Water Canon Salutation) toka kwa magari ya Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mara tu bada ya kuwasili  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016 Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ...

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Amjulia Hali Spika Mstaafu Samweli Sitta

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika Mstaafu, Samwel Sitta na mkewe Margaret wakati alipomjulia hali jijini Dar  es salaam Septemba 20, 2016.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).Chanzo Mpekuzi

Manispaa ya Kinondoni Yavunjwa Rasmi....Meya Boniface Kapoteza Nafasi Yake

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli amevunja Baraza la Madiwani rasmi baada ya serikali kuigawa manispaa hiyo kuwa mbili. Kagurumjuli alilivunja juzi saa 11:00 baada ya kumalizika kwa Baraza la Madiwani la kawaida. Alipokuwa akitangaza kulivunja baraza hilo, Kagurumjuli alisema amevunja baraza hilo kwa kuwa serikali imegawanya manispaa hiyo kuwa wilaya mbili, ya Kinondoni na Ubungo hivyo kwa kuwa wilaya zote tayari zina wakurugenzi, wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa wilaya imempasa kufanya hivyo. “Baraza la madiwani limevunjwa, kuvunjwa kwa baraza hili ni ukomo wa meya pia,” alisema. Aliongeza kuwa wiki ijayo kutakuwa na uchaguzi wa meya katika manispaa hizo. Meya wa Manispaa ya Kinondoni alikuwepo kabla ya kuvunjwa kwa baraza hilo ni Boniface Yakob ambaye amebaki nafasi yake ya udiwani. Kuvunjwa kwa baraza hilo kulikuwa kunatarajiwa baada ya serikali kugawanya manispaa ya Kinondoni kuwa mbili.Chanzo Mpekuzi.