Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2016

UMOJA WA VIJANA CUF WAMJIA JUU MTATIRO NA KAMATI YAKE.............//

JUMUIYA za Vijana wa Chama cha Wananchi ( CUF) katika mkoa wa Dar es Salaam, wameibuka na kulaani tabia ya inayojiita Kamati ya Uongozi ya chama hicho inayoongozwa na Julius Mtatiro, kutoa lugha za kubeza dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi. Vijana hao wamedai hatua hiyo ya Mtatiro na wenzake, kutumia vyombo vya habari hasa redio na televisheni, kumkashifu Msajili wa vyama kwa maamuzi yake ya kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kama mwenyekiti halali wa chama hicho kwa mujibu wa katiba, haikubaliki.JUMUIYA za Vijana wa Chama cha Wananchi ( CUF) katika mkoa wa Dar es Salaam, wameibuka na kulaani tabia ya inayojiita Kamati ya Uongozi ya chama hicho inayoongozwa na Julius Mtatiro, kutoa lugha za kubeza dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi. Vijana hao wamedai hatua hiyo ya Mtatiro na wenzake, kutumia vyombo vya habari hasa redio na televisheni, kumkashifu Msajili wa vyama kwa maamuzi yake ya kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kam...

Tundu Lissu akosekana Tena Mahakamani Kisutu, aibukia Mwanza ........//

Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, jana alishindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kujibu mashitaka ya uchochezi huku mdhamini wake akiieleza mahakama kuwa, yupo jijini Mwanza akisimamia kesi ya Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda katika Mahakama Kuu ya Mwanza. Lissu ambaye pia ni wakili wa Mahakama Kuu na mwansheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo anashitakiwa kwa uchochezi pamoja na washitakiwa wengine ambao ni ni Jabir Idrissa, mwandishi mwandamizi wa Gazeti la MAWIO, Simon Mkina, mhariri wa Gazeti hilo na Ismail Mehboob, meneja wa kampuni ya uchapishaji magazeti ya Flint. Mdhamini wa Lissu, Ibrahim Hemed, alitoa taarifa ya kutofika kwa mdhamana wake mahakamani hapo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba. Ibrahim alidai kwamba Lissu amempatia taarifa kuwa ameshindwa kufika kwa sababu yupo kwenye kesi ya uchaguzi huku Peter Kibatala wakili wa utetezi akiiomba mahakama ipokee taarifa za Lissu na ikubali kuhairisha kesi h...

Yahoo walichunguza barua pepe kwa niaba ya Marekani.............//

Yahoo walichunguza mamilioni ya barua pepe za watu kwa niaba ya serikali ya Marekani, ripoti ya shirika la habari la Reuters inasema. Shirika hilo la habari linasema kampuni hiyo iliunda programu maalum mwaka jana na kuitumia ili kutimiza ombi rasmi kutoka kwa serikali ya Marekani. "Yahoo ni kampuni inayofuata sheria, na hutii sheria za Marekani," kampuni hiyo imesema kupitia taarifa kwa BBC. Reuters wanasema maombi yalitoka kwa Shirika la Usalama wa Taifa (NSA) au kwa FBI. Programu iliyoundwa na Yahoo ilikuwa inachunguza uwepo wa tarakimu, alfabeti au ishara fulani za maandishi kwenye barua pepe zilizokuwa zikipokelewa. Yahoo yadukuliwa taarifa Udukuzi: Simu milioni 900 za Android hatarini Hata hivyo, Reuters wanasema hawakuweza kubaini ni habari za aina gani zilizokabidhiwa kwa maafisa wa Marekani au iwapo kampuni nyingine zinazotoa huduma mtandaoni zilihusika. Tuhuma hizo zinatokea chini ya wiki mbili baada ya kubainika kwamba wadukuzi waliiba mae...

Tyson: Ninatumia Cocaine kukabiliana na ugonjwa wa Kiakili......//

Bingwa wa ndondi katika uzani mzito duniani Tyson Fury amesema amekuwa akitumia Cocaine ili kumsaidia kukubiliana na matatizo ya kiakili. Bondia huyo wa Uingereza amesema kuwa amekuwa akiugua ugonjwa wa kiakili kwa miaka kadhaa na hajafanya mazoezi tangu mwezi Mei. Nimekuwa nje nikilewa ,Jumatatu hadi Ijumaa hadi Jumapili na kutumia Cocaine,Fury aliambia jarida la Rolling Stones. Hatua hiyo inajiri siku mbili baada ya Fury kudai katika mitandao ya kijamii kwamba amejiuzulu,kabla kukana madai hayo saa tatu baadaye akisema alikuwa akifanya utani. Akizungumza kuhusu maswala ya afya yake ,Fury aliongezea: Siwezi kukabiliana na matatizo haya na kitu kinachonisaidia ni wakati ninapokunywa ili nitoe matatizo hayo akilini.wanasema nina ugonjwa wa kiakili.Nahisi huzuni.Niingependa mtu aniue kabla sijajiua.BBC.

Kagame abadilisha baraza la mawaziri Rwanda.......//

Rais wa Rwanda Paul Kagame amefanya mageuzi madogo ndani ya baraza lake la mawaziri kwa kuunda wizara ndogo inayohusu maswala ya katiba na sheria nyingine. Mageuzi makubwa yanahusu wizara ndogo mpya iliyoundwa katika wizara ya sheria ikihusu maswala ya katiba na sheria nyingine. Wizara hiyo ndogo imepewa Bwana Evode Uwizeyimana ambaye wengi hapa Rwanda walimfahamu kama mkereketwa wa upinzani dhidi ya utawala wa RPF kabla ya kurejea nchini miaka 2 iliyopita akitoka uhamishoni nchini Canada. Mara tu baada ya kurejea nchini Bwana Uwizeyimana alijumuishwa katika tume ya Rwanda iliyofanya mabadiliko ya katiba ambapo rais Kagame aliongezewa muda wa kukaa madarakani. Mageuzi mengine yaliyofanyika siyo makubwa. Rais Kagame amembadilishia wizara Dr Diane Gashumba aliyekuwa waziri wa familia na usawa wa jinsia na kumweka katika wizara ya Afya,wadhifa uliokuwa wazi tangu kufutwa kazi kwa Dr Agnès Binagwaho miezi mitatu iliyopita. Aidha wizara ya maswala ya nchi za Afrika Ma...

Duterte asema Obama anaweza 'kwenda jehanamu'............//

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amerejelea tena shutuma zake dhidi ya Rais Obama na viongozi wengine wa nchi za Magharibi wanaopinga mpango wake wa kupambana na walanguzi wa dawa za kulevya. Kiongozi huyo amesema Bw Obama anaweza "kwenda jehanamu". Umoja wa Ulaya, ambao pia umemkosoa Bw Duterte, unaweza "kuchagua kwenda eneo la kutakasia dhambi ndogo, kwa sababu jehanamu kumejaa", amesema. Mfahamu rais Duterte, kiongozi aliyemtusi Obama Obama alipokutana na Duterte nchini Laos Duterte alinganisha vita vyake na vya Hitler Watu karibu 3,000 wameuawa tangu kiongozi huyo alipoingia madarakani mwezi Juni. Watu wanaoshukiwa kulangua mihadarati au kuwa waraibu wa dawa hizo wamekuwa wakiuawa na maafisa wa polisi na magenge yanayoungwa mkono na serikali. Bw Duterte amesema Urusi na China wako tayari kuwa washirika wake. Image copyright ...

China: 'Ukinunua iPhone 7 umejifuta kazi!'........//

Kampuni kadha nchini Uchina zimetoa onyo kali kwa wafanyakazi wake na kuwataka wasinunue simu mpya ya kampuni ya Apple, iPhone 7. Kampuni zilizotoa marufuku hiyo zinasema ni kwa sababu za kizalendo. Nyingine zimesema zinataka kuwafunza wafanyakazi wake kutopenda sana raha na anasa za dunia. Simu mpya ya iPhone 7 isiyotumia headphone Kampuni ya dawa ya Nanyang Yongkang Medicine, katika mkoa wa Henan, ni moja ya zilizoagiza wafanyakazi wake kutonunua simu za iPhone 7 au Iphone 7 Plus. "Ukivunja agizo hili, njoo moja kwa moja hadi afisini na utukabidhi barua yako ya kuacha kazi," ilani kutoka kwa kampuni hiyo iliyotumwa kwa wafanyakazi inasema. Image copyright Weibo Image caption Baadhi ya wafanyakazi wanasema barua ya k...

Antonio Guterres kuwa katibu mkuu mpya wa UN...........//

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Portugal Antonio Guterres anatarajiwa kuwa katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa UN ,kulingana na wajumbe wa umoja huo. Bwana Guterres mwenye umri wa miaka 66,''alipendelewa na wengi '',balozi wa Urusi katika umoja wa mataifa Vitaly Churkin alitangaza siku ya Jumatano. Kura ilio rasmi itafanyika katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi kuthibitisha uteuzi huo. Kiongozi huyo aliungwa mkono na mataifa yaliopo katika baraza la usalama la umoja wa mataifa Bwana Guterres ,ambaye aliongoza shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia wakimbizi kwa kipindi cha miaka 10 atachukua mahala pake ban Ki-moon mapema mwaka ujao....