Skip to main content

Posts

MBABE WA BALON`DOR AFRIKA(GEORGE WEAR) ATAKA URAIS LIBERIA MWEZI OKTOBA. Bofya picha hii

Baada ya kuongoza kwa mwongo mmoja kama rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, atastaafu baada ya uchaguzi mkuu nchini humo mwezi Oktoba. Orodha kamili ya wanaowania kumrithi mshindi huyo wa Tuzo ya Amani ya Nobel sasa imejulikana, shirika la habari la AFP limeripoti. Kuna jumla ya wagombea 20. Miongoni mwa wagombea hao ni nyota wa zamani wa soka George Weah, ambaye alishindwa na Johnson Sirleaf uchaguzi wa mwaka 2005. Jewel Howard-Taylor, 54, mke wa zamani wa Charles Taylor atakuwa mgombea mwenza wa Bw Weah. Mbabe wa kivita wa zamani Prince Johnson pia anataka kuongoza taifa hilo. Shirika la habari la AFP linasema kuna mwanamke mmoja pekee aliyejitokeza kuwania, MacDella Cooper, ambaye alikuwa mwanamitindo lakini kwa sasa ni mfanyakazi wa hisani. Makamu wa rais wa Johnson Sirleaf, Joseph Boakai, pia anawania katika uchaguzi huo utakaofanyika tarehe 10 Oktoba mwaka huu. BBC

SANCHEZ AOMBA KUONDOKA ARSENAL.!Tazama hapa alichokisema kuhusu kuondoka kwake.

Muda mwingine waungwana wakizungumza hutumia tafsida ili kupunguza ukali wa maneno na nadhani Sanchez ni muungwana kwani amesema anataka kuondoka Arsenal lakini ameongea maneno hayo kwa tafsida. Sanchez na Arsenal bado hakijaeleweka na nyota huyo hadi sasa hajasaini mkataba mpya huku kocha wake mzee Wenger akisema nyota huyo hana mpango wa kuondoka na inambidi abaki kwa kuwa ana mkataba na timh hiyo. Sanchez alizisikia taarifa za babu Wenger bila shaka na yeye kaja na lake ambalo ni tofauti na la babu Wenger kwani haihitaji akili ya darasa la saba kujua kwamba Sanchez haitaki tena Arsenal na anataka kuondoka. “Mimi tayari nimefanya maamuzi lakini kawaida maamuzi ni ya pande mbili kwahiyo bado nawasikiliza wao lakini iko wazi msimu ujao nataka kucheza katika Champions League na kushinda mashindano hato ni ndoto yangu kubwa” alisema Sanchez. Arsenal hawapo katika mashindano ya Champions League msimu ujao,Arsenal hawajawahi kubeba kombe la Champions League na hawatabi...

TETESI ZA SOKA MAJUU LEO JUMA PILI JULAI 16 2017.!Bofya picha hii kutazama tetesi zote.

Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday) Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport) Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday) Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror) Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Da...

BAADA YA KUMWAGIA FEDHA,MAYWEATHER AMUONESHA McGREGOR SAA YA Tsh.3bilio.Bofya picha hii.

Baada ya kummwagia fedha walipokuwa New York bado Mayweather hakumuacha salama McGregor walipokutana tena SSE Arena, Wembley, London mara hii akimtambia kwa kumuonesha saa yenye thamani ya dollar 1.4 milioni (£1.06m), ambazo ni zaidi ya Tsh. 3 bilioni. Hatua hiyo ilikuja baada ya  Conor McGregor kumwambia Mayweather kuwa amevaa high heels walipokuwa kwenye ziara London kuelekea pambano lao.   Tunahesabu siku 40 kuanzia leo ili kuifikia August 26 tarehe ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mchezo wa ngumi duniani kote kushuhudia pambano kati ya  Floyd Mayweather vs Conor McGregor litakalopigwa  T Mobile Arena, Las Vegas ambapo Mayweather atavuna paundi 78m sawa na Tsh. 228.3 Bilioni.

DONE DEAL: CHELSEA WAMEKAMILISHA USAJILI WA MLINZI WA UJERUMAN.! Bofya picha hii.

Mabingwa wa Premier League, Chelsea FC wamekamilisha usajili wa mlinzi wa timu ya Taifa la Ujerumani Antonio Rudiger kutoka Klabu ya FC Roma ya nchini italia(serie A) kwa dili lenye thamani ya pound 31m ambayo inaweza kuongezeka hadi pound 35m. Antonio Rudiger mwenye umri wa miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitano kutumika Stamford Bridge baada ya kufanya vipimo vya afya Jumapili.

DAH! SHABIKI WA SUNDER LAND BRADLEY LOWERY ALIYEGUSA NYOYO ZA WENGI AAGA DUNIA!!

Shabiki wa klabu ya Sunderland wa umri wa miaka sita Bradley Lowery, ambaye tatizo lake la kiafya liligusa nyoyo za wengi amefariki dunia. Bardlaye alikuwa anaugua ugonjwa ambao wa Kiingereza hufahamika kama neuroblastoma - aina nadra ya saratani - tangu alipokuwa na umri wa miezi 18. Bradley alifanywa kuwa kibonzo-nembo wa klabu hiyo na akaunda urafiki wa karibu na mshambuliaji wa klabu hiyo Jermain Defoe. Aidha, aliongoza wachezaji wa England kuingia uwanjani Wembley wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania. Kifo chake kimethibitishwa na wazazi wake kwenye mitandao ya kijamii. "Kijana wetu mkakamavu ameenda kuwa na malaika leo. "Alikuwa shujaa wetu na alipigana sana lakini alihitajika kwingine. Hatuna maneno ya kueleza jinsi tulivyohuzunishwa na kifo chake." Bradley alipewa matibabu lakini saratani yake ikaibuka tena mwaka jana. Wahisani walichangisha zaidi ya...

SIWEZI KUBADILI JINA LANGU KWASABABU YA CHID BENZ: CHIN BEES.

Msanii wa Bongo Fleva, Chini Bees amesema hawezi kubadilisha jina ili kumkwepa Chid Benz. Wiki iliyopita rapper Chid Benz alimtaka msanii huyo kubadili jina kwa sababu yanafanana kitu ambacho Chin Bees amekuja kukupinga. “Mimi siwezi kubadilisha jina kwa sababu ya Chid Benz kwa sababu halifanani, very different. Mimi nafanya muziki wangu, siwezi nikakaa nipiganie jina, hivyo bro kama anahitaji jina dah!, sidhani kama jina langu linaendana na lake  me am do my thing,”  Chin Bees amekiambia kituo kimoja cha Television nchini. Sababu ya Chid Benz kumtaka Chin Bees kubadili jina alidai kwanza yamefanana na pili yeye ana hit song song 32 huku akiadai C. Bees hana hata nyimbo saba, hivyo hawafanani.