Msimu mpya wa soka barani Ulaya unatarajiwa kuanza rasmi leo wakati utakapopigwa mtanange utakaowakutanisha wababe wa ulaya msimu uliopita. Mabingwa wa Champions League Real Madrid na mabingwa wa Europa Cup Manchester United. Mchezo huu utapigwa nchini Macedonia mashariki mwa bara la ulaya, kuanzia majira ya 9:45 usiku. Mchezo huu unakutanisha miamba mikubwa ya soka barani ulaya siku chache baada ya kukutana nchini Marekani katika mechi za maandalizi ya msimu mpya. Cristiano Ronaldo amerejea mazoezini wiki iliyopita na leo ametajwa katika kikosi kinachosafiro kuelekea Macedonia kwa ajili ya mchezo huo, United watamkosa Eric Bailly pamoja na Phil Jones wenye adhabu za kufungiwa mechi kutokana na makosa ambayo waliyatenda msimu uliopita. Kwa kuanzia kuuchambua mchezo huu tuanze kuangalia takwimu mbalimbali zinazohusisha mchezo wa UEFA Super Cup tangu ulipoanzishwa kuchezwa mnamo mwaka 1973. Champions League vs UEFA Cup Winners • Mabingwa wa Champions League wames...