Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki (EALS) kimemwandikia barua Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe kikimtaka aache kuingilia uchaguzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS). Barua hiyo imekuja baada ya Dkt. Mwakyembe kudaiwa hivi karibuni kutishia kuifuta TLS kwa madai kwamba imeanza kuingiliwa kisiasa. Barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na Rais wa EALS, Richard Mugisha, inasema TLS si chama cha kisiasa na kimeanzishwa kwa kufuata sheria zote. “Mheshimiwa Waziri, tumesikitishwa na taarifa ambazo zimeenea kwenye vyombo vyote vya habari na gazeti la East African la Februari 18 ambalo limekunukuu ukisema kwamba Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kina muingiliano wa kisiasa,” inasema sehemu ya barua hiyo. Katika barua hiyo, Mugisha anasema wanasheria wanatakiwa wapewe uhuru, wasiingiliwe na serikali kama ilivyo kwa nchi nyingine kwani kuingilia ni sawa na kuvunja sheria za nchi. Rais wa sasa wa TLS, John Seka amesema kuwa cham...